Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ya kuwasaka wote waliotelekeza familia zao imeanza kuzaa matunda mara baada ya mtu mmoja kukamatwa na jeshi la polisi.

Mtu huyo anayejulikana kwa jina la Frank Eliah alikamatwa mara baada ya mke wake aliyezaa naye, Halima Hussein kufikisha malalamiko kwa Mkuu wa Mkoa kuwa ametelekezwa na mume wake.

Amesema kuwa alifikia uamuzi wa kwenda kwa mkuu huyo wa mkoa mara baada ya mumewe kugoma kutoa hela ya matumizi ya mtoto.

Kwa upande wake, Frank Eliah ambaye ni mume wa Halima Hussein amesema kuwa huwa anapeleka matumizi kwa mama huyo lakini huwa hayatoshelezi kwa kuwa kipato chake ni kidogo.

 

Urusi yaionya Marekani, yaapa kulipiza shambulio lolote
Video: TAMWA wampongeza Makonda

Comments

comments