Timu ya taifa ya vijana chini ya Umri wa miaka 17(Serengeti Boys) leo imeitembelea kampuni ya simu Airtel ili kujifunza mambo mbalimbali ambapo ni pamoja na kuwatia moyo na kuwajenga kisaikolojia wachezaji kufuatia mechi inayowakabili siku ya jumapili.

Kampuni ya Airtel Imeialika timu hiyo sababu Kubwa ni kutaka kuendelea Kuisaidia kwani vijana wengi waliopo kwenye kikosi hicho cha Vijana kimetokana na Mashindano ya Airtel rising star yanayodhaminiwa na Airtel.

Aidha Airtel kupitia kwa Afisa Uhusiano kampuni hiyo bw,Jackson MMbando alisema ‘’Wataendelea kuisaidia timu hiyo na kwamba hiyo ndio hazina ya baadae,kwani kila kitu kizuri huandaliwa na baadae kuanza kula matunda.

Naye  mwenyekiti wa soka la vijana kuoka TFF bw,Ayoub Nyenzi aliwasilisha mahitaji ambayo wanahitaji kusaidiwa na kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuilea na kusismamia shughuli zake.

Kwa upande wake kocha wa timu hiyo Bw,Bakari Shime alisema Wamejipanga vizuri kuweza kuwakabili wapinzani wao kutoka Schelles na kwamba Watanzania wajiandae kupokea ushindi.

Majina ya Waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha 5 haya hapa
TFF Yajisafisha Kwa Kutoa Ufafanuzi