Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia kitengo cha uthamini imeto taarifa ya utaratibu wa fidia wa mali isiyohamishika kama ardhi, majengo, mazao, pia zinazohamishika kama vile samani za mashine, magari na vifaa mbalimbali na kuongeza kuwa zipo aina kuu mbili za uthamini ambazo ni uthamini wa ujumla, kawaida na uthanimi wa kisheria .
Hayo yamesemwa na kaimu mthamini mkuu wa serikali Evelyne Mugashwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo,na kuongeza kuwa uthamini wa fidia ni malipo yanayotolewa kwa waathirika kwa mtu au taasisi kama mbadala wa mali yake kutokana na kuondolewa kwenye eneo lake lililotwaliwa kwa manufaa ya umma na kupangiwa matumizi mengine.
Mugashwa amesema kuwa uthamini hufanywa na mthamini kulingana na misingi ya taaluma ya uthamini na hufanyika kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya vijiji Na.5 za mwaka 1967.