Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala (UVCCM), Augustino Matefu amesema kuwa mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe ameishiwa mbinu mpya za kuibua hoja.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa mbunge huyo amekuwa akidandia kila hoja inayojitokeza mbele yake.

Akizungumzia sakata la Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali, Matefu amempongeza Prof. Mussa Assad kwa kuonyesha dalili za kuitikia wito wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Aidha, Matefu amewashukia mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume kwa kuligeuza sakata la CAG kuwa la kisiasa.

“Kuna watu wanafanya makusudi kuipotosha jamii kuhusu sakata hili la CAG, wanakimbilia mahakamani wakati wanajua kabisa kwamba sheria imefafanua vizuri kuhusu suala hili,”amesema Matefu

'Serikali' ya Burkina Faso yajiuzulu
66 wafa Mexico mlipuko bomba la mafuta

Comments

comments