Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole ametoa mchanganuo wa jinsi Trilioni 1.5 zilivyotumika.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kurudi darasani kwa ajiri ya kujifunza hesabu.

Amesema kuwa kuna mambo mengi ya hesabu ambayo Mbunge huyo hayafahamu hivyo hatakiwi kukurupuka kutoa takwimu ambazo zinawavuruga Watanzania.

“Huyu Zitto amekuwa akibeza kila kitu ambacho kimekuwa kikifanywa na serikali, sijui anataka kifanyike kipi, haya ni mawazo ya kishetani, huwezi kuongea kwa kukurupuka, huu ndio ukweli niliouweka wazi, Zitto rudi darasani hujui hesabu,”amesema Polepole

 

Diamond ampa tano Ali Kiba, Esma ataka aige mfano wake
Video: Matibabu ya Lissu yawaumbua Chadema bungeni, Mtifuano wabunge Makonda