Taarifa mpya iliyotolewa baada ya uchunguzi wa awali juu ya chanzo cha vifo katika tamasha la Muziki la Travis Scott zinasema kuna mtu mmoja miongoni mwa waliohudhuria alirukwa na akili na kuanza kuwachoma watu Sindano yenye kuaminika kwamba ilikuwa na chembe za madawa ya kulevya.

Jambo hilo ndilo lililokuwa chanzo cha kuibua zogo kiasi cha watu wengi kuanza kusukumana, kitendo kilichopelekea watu kuanza kukanyagana, kubanana kiasi cha wengine kukosa pumzi na kufariki huku wengime kadhaa kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa TMZ  inasemekana baadhi ya watu walipatikana wakiwa wamefariki kwa kile kinachodaiwa kuwa walipatwa na shambulio la moyo kitu kinachopelea kuhisiwa kwamba pengine  walichomwa sindano na mtu huyo.

Aidha Travis Scott  ametoa kauli rasmi kufuatia tukio hilo kwa kuweka bayana kuwa ameshtushwa sana na tukio hilo na anatoa pole kwa familia za wahanga wa tukio hilo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 7, 2021
Ummy Mwalimu aagiza mchakato wa ujenzi na ukarabati wa soko la Kariakoo uanze