Vigogo wa IPTL, James Rugemalila na mmiliki wa Kampuni ya PAP, Harbinder Seth Singh wamepandishwa mahakamani kwa makosa la kuhujumu uchumi wa nchi kwa kipindi kirefu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kamishna Valentino Mlowola alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa TAKUKURU imechunguza shauri hilo la kesi ya Escrow na Kampuni ya kufua umeme Independent Power Tanzania Limited IPTL kwa muda mrefu hivyo kujiridhisha kuwa watuhumiwa hao wana kesi ya kujibu hivyo kuamua kulipeleka mahakamani.

“Kwa hatua ya awali watapelekwa Mahakama ya Kisutu, baada ya hapo taratibu za kimahakama zitafuata kwa kuwapeleka mahakama maalumu kutokana na kiwango cha hujuma kilichofanyika na fedha zilizohusika,”amesema Mlowole

Hata hivyo, ameongeza kuwa ni siku nyingi amekuwa akiulizwa maswali kuhusu kesi ya Escrow na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL hivyo muda muafaka umefika wa kuweza kushughulikiwa kwa kesi hizo.

Paolo Maldini Kuwakabili Nadal, Federer, Djokovic
Katy Perry afikisha wafuasi milioni 100 twitter

Comments

comments