Vijana wa Chama Cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kinondoni wamemchukulia fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba.

Hayo yamejiri leo Julai 23, 2020 huku wakisema wana imani katika wagombea wote wa upinzani ambao wamepitishwa na vyama vyao kuwania nafasi ya Urais hawamuwezi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM isipokuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Ilala, Salim Muslim amesema jumuiya ya vijana imefikia uamuzi huo baada ya kutafakari na kuona kiongozi huyo anazo sifa za kugombea nafasi Urais kutokana na ubobezi katika masuala ya uchumi.

Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Mkiti wa chama hicho Taifa prof. Lipumba amesema aliamua kukaa kimya ili kutoa nafasi kwa wanachama wengine wajitokeze kuchukua fomu ili kupambana ambapo amesema yapo mengi ambayo kama Chama wanaamini bado ni matakwa ya wananchi na hayajatekelezwa na serikali.akiahidi endapo atapata ridhaa ataunga serikali ya Umoja wa kitaifa ikiwemo kukamilisha mchakato wa katiba mpya.

Katibu wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni, Suleiman Masauni amewataka wanachama wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Urais kujitokeza na kuchukua fomu ambazo gharama yake ni shilingi laki 5.

Kwa mujibu wa chama hicho kesho Tarehe 24 July ndiyo siku ya mwisho ya kurejesha fomu ya wagombea kwa ngazi ya Urais hivyo atalazimika kuijaza fomu hiyo kwa kuwa vijana wa Chama Cha CUF wameonesha Imani kubwa Kwake kuwa anaweza kuwavusha.

Tayari tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshatangaza tarehe ya kuanza kampeni ambayo ni Agosti 26 na uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba 28 mwaka huu.

TANZIA: Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa afariki dunia, Rais Magufuli atangaza maombolezo siku 7
NEC yatoa ratiba fomu za Urais, Jimbo la Chilonwa laitwa Chamwino