Zaidi ya wanawake 200 nchini Kenya wenye umri hadi miaka 105 wamekuwa wakipewa mafunzo ya kujihami dhidi ya ubakaji unaofanywa na vijana wenye umri mdogo, tangu mwaka 2007.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na mtandao wa Reuters, mwanamke mmoja kati ya wanne hufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono katika eneo la Korogocho, ambalo ni eneo hatari la uswahilini.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa wastani wa wanawake wazee watatu walikuwa wakibakwa na vijana katika eneo hilo kila mwezi, na wengine wakibakwa na kundi la vijana hadi kufa, hali iliyosababisha raia mmoja wa kigeni pamoja na mkewe kuanzisha darasa la mafunzo ya kujihami kwa wanawake na wazee hao.

“Darasa linazidi kukua, sasa ni zaidi ya madarasa saba,” alisema Jake Sinclaire, Mmarekani aliyeanzisha mradi wa mafunzo hayo kwa wanawake akiwa na mkewe Lee miaka kadhaa iliyopita baada ya kusikia masimulizi ya kutisha ya ubakaji wa vikongwe katika eneo la Korogocho.

“Baadhi ya vijana wa eneo hili wanafuata imani potofu kuwa baada ya kufanya unyang’anyi, wakilala na vikongwe au wanawake wenye umri mkubwa sana wanakuwa wametakasika,” aliongeza.

Akizungumzia mafunzo wanayoyatoa tangu mwaka 2012, ni pamoja na namna vikongwe wanavyoweza kujihami dhidi ya wabakaji kwa kuvuruga kwa kuwachoma machoni, kuwachanganya kwa kugeuka kichaa na kuwavaa kabla hawajataka kuwagusa.

“Unafanya kama kichaa na unamfuata anayetaka kukushambulia. Unamtisha kwa sababu unakuwa sio mtu aliyekuwa anategemea,” alisema Jacqueline ambaye ni moja kati ya wakufunzi.

  • Ajali mbaya ya basi yatokea nchini Uganda
  • Kampeni hiyo pia imesaidia kuzaliwa kwa mradi wa kuwafunza wanafunzi wa shule za Sekondari katika eneo hilo ambapo maelfu wanapatiwa mafunzo dhidi ya unyanyasaji wa kingono. Programu hiyo inaitwa ‘No Means no World’.

Chanzo: Reuters

Waziri afanya ziara ya kushtukiza Uwanja wa ndege
Video: Itazame ngoma mpya ya Belle 9