Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa chama hicho kutokuwa na majina yao mfukoni katika mchakato wa kura za maoni kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge.

Rais Mgufuli ametoa onyo hilo leo, Januari 24, 2020 jijini Dar es salaam alipokutana na viongozi wa mikoa, wilaya na jumuiya za chama hicho kutoka mikoa yote nchini.

Amesema viongozi hao wanatakiwa kuweka mbele maslahi ya chama hicho kwa kuchagua wagombea wenye sifa na wanaokubalika na wananchi kwani ndani ya CCM kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.

“Wakati wa mchakato wa uchaguzi, tusiende na majina mfukoni, kwamba huyu ni wa mwenyekiti, huyu ni wa katibu, wakati mwingine unakuta mwenyekiti na katibu mkuu wanagombana, tuweke maslahi ya chama chetu mbele” amesema Rais Magufuli.

Aidha amewataka viongozi hao kuhakikisha wanadumisha uhusiano kati yao na viongozi wa Serikali ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kama ilivyopangwa na kuahidiwa kila sehemu.

Magufuli aruhusu makontena ya Makinikia yaliyozuiwa 2017 yauzwe
Hukumu yatolewa kwa watanzania waliozamia Afrika kusini