Wabunge wanne waliokuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baadaye kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushinda nafasi zao za ubunge wameapishwa leo bungeni na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kuanza kuzitumikia nafasi hizo tena kupitia chama tawala.

Miongoni mwa wabunge hao walioapishwa ni Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Milya, Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi pamoja na Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba.

Aidha, wabunge hao walikuwa ni wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakihudumu kwenye chama hicho kwa kipindi cha miaka 2 na nusu, lakini baadaye walihama kutokana sababu mbalimbali ikiwemo kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewapongeza wabunge hao na kuwataka kutekeleza majukumu yao ya kihalali ya kuishauri serikali.

 

Mawaziri wenye mahudhurio hafifu bungeni watajwa
Waziri wa Ulinzi wa Israel ajiuzulu

Comments

comments