Wanaume wawili nchini Indonesia wamechapwa viboko 85 kila mmoja mara baada ya kufumaniwa wakifanya mapenzi ya jinsia moja ambapo kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo ni makosa makubwa.

Aidha, katika utekelezaji wa adhabu hiyo, wanaume hao walipandishwa jukwaani kisha kuvalishwa mavazi meupe maalumu kwaajili ya adhabu kisha kuanza kuchapwa viboko na kundi la watu waliokuwa wamefurika katika eneo hilo.

Indonesia imeharamisha mapenzi ya Jinsia moja kwa kutunga sheria kali za kukabiliana na watu wanaojhusisha na mapenzi ya jinsia moja kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya dini na utamaduni wa nchi hiyo.

 

Hata hivyo, Sheria kali dhidi ya mapenizi ya jinsia moja zilipitishwa mwaka 2014 na kuanza kufanya kazi mwaka 2015 huku hukumu za kuchapwa viboko hadharani zikiwa ni za awali.

Basata Wamsaka Ben Pol kuhusu picha alizopiga akiwa ‘mtupu’
Griezman kung'oka Atletico Madrid