Viongozi vya vyama vya upinzani waliowahi kujiapisha Barani Afrika inazidi kuongezeka mara baada ya jana kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga kujiapisha.

Odinga siyo mtu wa kwanza kufanya kitu kama hicho, kwani kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye alifanya hivyo baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Aidha, Etienne Tshisekedi alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Sese Seko wa Zaire, DRC, na baadaye Laurent Kabila.

November 2011 Tshisekedi aliposhindwa katika uchaguzi dhidi ya mtoto wa Laurent Kabila, Joseph Kabila ambaye ndiye rais wa sasa aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha katika uwanja wa Wahanga Kinshasa kutibuka.

Moshood Abiola, Baada ya kutembelea nchi nyingi za Magharibi kutafuta msaada ili kumkabili aliyekuwa Rais wa Nigeria, Sani Abacha katika utawala wake, Moshood Abiola alijitangaza mwenyewe kuwa rais wakati Rais Abacha bado yupo madarakani.
Hata hivyo, Jean Ping kiongozi wa upinzani Gabon mwaka 2016 alijitangaza mwenyewe kuwa rais na kutoa wito kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Rais Ali Bongo alikuwa ameshinda.
Diwani alalamikia kundi la Fisi
Familia ya Lissu yaicharukia Bunge

Comments

comments