Shule zimefungwa nchini Pakistan huku barabara zikiwa tupu wakati makundi ya Kiislamu ya itikadi kali yakiendelea na maandamano ya kupinga uamuzi wa kuachiwa kwa mwanamke wa Kikristo aliyehukumiwa kifo kwa kukashifu dini.

Jeshi la polisi nchini humo limesema kuwa wafuasi wa mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali walifunga mojawapo ya barabara kuu za kuingia mji mkuu Islamabad, huku wakiwalazimisha wasafiri kutumia njia nyingine mbadala, huku watu wengi wakiamua kubaki majumbani mwao ili kuepuka maandamano hayo.

Aidha, maandamano hayo yalizuka mara baada ya jopo la majaji watatu kuamuru kuachiwa huru kwa Asia Bibi mwanamke wa Kikristo aliyehukumiwa kifo mwaka wa 2010. uamuzi huo umesifiwa kuwa wa kihistoria na wanaharakati wa haki za binaadamu.

Wafuasi wa vuguvugu la Kiislamu wa Tehreek-e-Labaik – TLP waliandamana katika miji yote na viongozi wake wakaapa kuendelea na maandamano yao.

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Imran Khan ametoa wito wa kuwepo utulivu na kuwaonya viongozi wa maandamano kupitia hotuba yake kupitia televisheni ya taifa juu ya kutoishambulia serikali.

 

Kocha Scaloni amkumbuka Erik Lamela
Video: Magufuli aanika utajiri Tanzania, Mbowe azidiwa...