Nchini Rwanda, wakimbizi takribani 700 wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), kutoka kambi ya Kiziba wameandamana nje ya ofisi ya UNHCR kupinga kupunguzwa kwa mgao wa chakula kwa asilimia 25.

Kufuatia maandamano hayo wakimbizi watano wa DRC, wamauawa na wengine akiwemo afisa wa polisi kujeruhiwa.

”Tulitumia nguvu za kadri ambazo zilipelekea watu 20 waliokuwa wanaleta vurugu na maafisa polisi kadhaa kujeruhiwa. Wote hao walipelekwa hospitali mara moja. Bahati mbaya watu watano kati ya wale waliokuwa wanaleta vurugu walipoteza maisha kutokana na majeraha hayo.” Tamko la polisi.

Polisi wamesema wamewakamata wakimbizi 15, kwa tuhuma za kuandaa maandamano kinyume cha sheria, kuwateka watu na kuchochea vurugu.

Wakimbizi wanasema idadi ya vifo inaweza kuwa iko juu kuliko ile iliotolewa na polisi.

Hata hivyo Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR limesema limeshtushwa na taarifa za vifo vya wakimbizi hao nchini Rwanda.

 

Msemaji wa UNHCR, Cecile Pouilly, amewataka wahusika nchini Rwanda kuhakikisha usalama wa wakimbizi baada ya maandamano yaliyokuwa yakiendelea tangu Febuari 20 kusababisha vifo na majeruhi.

Rwanda inawahifadhi zaidi ya wakimbizi 173,000 katika kambi sita, ikiwemo ya Kiziba ambapo baadhi ya Raia wa Congo ambao wameishi zaidi ya miaka 20.

 

Korea Kaskazini yaikaribisha Marekani mezani
Mkuu wa Jeshi la Korea Kaskazini atua Korea Kusini