Vijana 3 waliokuwa waliokuwa wamepotea Visiwani Pemba wamekutwa katika maeneo mawili tofauti na kuokotwa wakiwa hoi na Wasamaria wema maeneo ya Wete Visiwani Pemba na kupelekwa Hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma za matibabu.

Vijana hao waliopotea kwa zaidi ya siku 12 ni, Thuwein Nassor Hemed ( 30), Khamis Abdalla Matter (25), Khalid Khamis Hassan. (30) wameokotwa wakiwa katika hali mbaya, wawili kati yao wameokotwa katika eneo la Mzambarau Takao, Jimbo la Mtambwe usiku wa manane huku wakiwa wamefungwa vitambaa usoni, na mwingine kaokotwa Likoni jimbo la Kojani.

Mbunge wa jimbo la Mtambwe, Khalifa Mhamed Issa ambae aliliacha Bunge na Kurudi jimboni kushirikiana na Wananchi wake waliwachukua vijana hao na kuwapeleka hospitali baada ya kupata pf3 ya polisi.

 

Mkurugenzi Halmashauri ya Kongwa afariki dunia
Tanzania yapanda nafasi 9 viwango vya FIFA

Comments

comments