Kambi rasimi ya upinzani imegoma kusoma maoni yake kuhusu muswaada wa marekebisho wa sheria mbalimbali baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuagiza kuondolewa kwa baadhi ya maneno katika hotuba hiyo.

Msemaji wa Kambi hiyo, Ali Saleh alizuiwa kusoma kifungu kinachotoa wito wa kuundwa Tume ya Kimahakama kuchunguza mashambulizi dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Aidha, Ali Saleh alisoma maoni hayo kwa niaba ya Msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu aliyeko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Hata hivyo, Baada ya kauli hiyo, Saleh amesema upinzani unaiamini na unaisimamia hotuba hiyo kwa kuwa Wabunge wote wanayo nakala yake, na kisha kuomba kuiwasilisha.

 

Putin: Hatima ya Wasyria iko mikononi mwao
Azam FC yaichakaza Shupavu FC