Waganga wawili wa tiba mbadala na watu wengine watano wanashikiliwa na polisi Wilayani Igunga mkoa wa Tabora, kwa tuhuma za kupiga ramli chonganishi na kuchoma moto nyumba tatu

Kutokana na kitendo hicho, familia za nyumba zilizochomwa zimekosa makazi na kuhifadhiwa na wasamalia wema.

Hayo yamethibishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi, Willibrod Mutafungwa, ambapo amewataja wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni waganga Chemani Ndishiwa (79) na Nzali Mayunga (40). Wengine ni Masanja Seni (65), Kasura Msomi (31), Michael James (19), Dotto Lukelesha (41) na Samuel Jonas (18), wote wakazi wa Kijiji cha Mwakwangu Kata ya Igurubi.

Mutafungwa amesema kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne majira ya usiku katika kijiji cha Mwakwangu na kuwa baadhi ya wananchi walikwenda kwa waganga hao wawili kupiga ramli na kuambiwa kwamba katika kijiji hicho, kuna baadhi ya familia ni wachawi.

Kwa mujibu wa Mutafungwa, baada ya kuelezwa hivyo, ndipo waliamua kukodi vijana kwa kuwalipa fedha ambazo hata hivyo, kiasi chake hakukitaja na ndipo vijana hao walikwenda hadi kwenye nyumba ya Luli Lukeresha na kuchoma makazi yake.

 

 

Polepole ashangazwa ACT-Wazalendo kuendeshwa mtandaoni
Siwezi kwenda mafichoni, nitarudi Tanzania- Lissu

Comments

comments