Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali inaendelea kufanya uchambuzi wa kubaini watumishi wote waliostaafu kabla ya 1999 ambao walikuwa wakichangia katika mifuko ya hifadhi ya Jamii ili waweze kulipwa madai yao ambapo mpaka sasa ni shilingi Bilioni 150 zimeshalipwa.

Akizungumza na watumishi wa Chama cha Walimu Tanzania CWT kwa niaba ya Waziri Mhagama, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge kazi ajira na Vijana, Anthony Mavunde amesema ni dhamara ya Serikali kuhakikisha wastaafu wote wakiwemo walimu wanalipwa madai yao.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Walimu Tanzania CWT, Leah Ulaya amesema changamoto kubwa wanayokabiliwa nayo  ni baadhi ya vyama vinavyopingana na CWT kuleta mgogoro ndani ya chama hali inayofanya wanachama kushindwa kupata haki zao.

Naye katibu Mkuu wa CWT Taifa Mwalimu Deus Seif amesema kuwa walimu wanakabiliwa na Changamoto mbalimbali ambazo zinapelekea baadhi ya walimu kutotekeleza majukumu yao vyema.

Hivyo wameiomba Serikali kuipa kipaumbele kada hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Nape ajilipua tena, ‘nyekundu iwe nyekundu’
Man Utd wamekubali kumuachia Daley Blind

Comments

comments