Wakati kikosi cha Mbeya City FC kikitarajiwa kushuka ndimbani  hapo kesho kucheza mchezo namba 98 wa ligi  kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Majimaji FC ya Songea kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,taarifa  imetolewa  kuwa nyota watatu  kikosini wataukosa mchezo huo.

Muda  mfupi uliopita afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten, amesema nyota watatu Ayoub Semtawa,John Kabanda na Omary Ramadhani hawatakuwa sehemu ya mchezo huo kwa sababu ya kupisha majeraha walioyapata kwenye michezo mitatu ambayo City ilicheza ikiwa nje ya uwanja wa nyumbani (Sokoine).

“Nimezungumza na dakatari wetu leo asubuhi, amenifahamisha kuwa hakuna uwezekano wa kuwatumia wachezaji Ayoub Semtawa, Omary Ramadhani na John kabanda kwa sababu bado hawajapona majeraha yao waliyoyapata kwenye michezo yetu iliyopita,kulikuwa na dalili na kupona kwa Omary lakini taarifa ya dakatari ndiyo hiyo hakuna uwezekano huo kwa sasa,” alisema.

Akiendelea zaidi, Ten alisema, Ayoub semtawa aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya African Lyon atalazimika kukaa nje kwa wiki tatu zaidi kabla ya kurejea uwanjani huku Kabanda na Omary wanaweza kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa tarahe mbili dhidi ya Young Africans.

“Tunaweza kuwatumia Omary na Kabanda kwenye mchezo ujao lakini hakuna uwezekano wa Semtawa kurejea uwanjani kwa sasa, daktari amesema atalazimika kukaa nje kwa majuma matatu zaidi hii ni kwa sababu alichanika nyama za paja ambazo zinahitaji muda kidogo wa mapumziko kabla ya kurejea”.

Katika hatua nyingine Ten aliweka wazi kuwa walinzi, Hassan Mwasapile na Haruna Shamte waliokuwa nje kwa majeraha tayari wamerejea kikosini na wamekuwa sehemu ya kikosi kwenye mazoezi ya siku tano yaliyofanika kwenye uwanja wa Sokoine kujiandaa na mchezo wa kesho hivyo hakuna shaka yoyote kuwa wanakuja kuimarisha safu ya ulinzi ya City.

“Taarifa nzuri kikosini ni kuwa Hassani Mwasapile na Haruna Shamte wanarejea kikosini, hili ni jambo jema kwa saababu wanakuja kuimarisha safu yetu ya ulinzi katika kuhakikisha tunaibuka na ushindi, uwepo wao utampa nafasi nzuri kocha wetu Kinnah Phiri kupanga kikosi ambacho  kitampa matokeo”, alimaliza.

Mashabiki Wa Chelsea FC, West Ham Utd Kuchunguzwa
Pep Guardiola Amfukuza Sergio Aguero Man City