Watoto nane wameokolewa wakiwa hai kati ya 12 waliokwama ndani ya pango lililojaa maji huko nchini Thailand,huku jitihada za uokoaji zikiwa zimesitishwa kwa muda katika kazi hiyo inayotajwa kuwa ni hatari kwa waokoaji pia kwani tayari mzamiaji mmoja amefariki dunia.

Wazamiaji kutoka nchi mbalimbali wamewasili Thailand kusaidia kazi hiyo, huku wazazi wa watoto hao wakiwa katika hali ngumu na kuomba kila linalowezekana lifanyike kunusuru maisha ya watoto wao.

Aidha, Watoto hao wa kiume walikwama mapangoni humo tangu June 23 huku uokoaji wao ukiwa ni wa hatari na wenye vikwazo vingi kwa maisha ya waokoaji.

Hata hivyo, Awamu nyingine ya uoakoji watoto hao na kocha wao walioingia ndani ya pango hilo kufanya utalii inatarajiwa kuanza tena leo siku ya Jumatatu ambapo kazi hiyo ilisimamishwa kwaajili ya maandalizi Zaidi ya vifaa vya hewa.

Young Killer afunguka mpango wa kuuza msemo ‘Pambana na Hali Yako’
Neymar alia na kipigo cha Ubelgiji, ajiuliza kurejea PSG

Comments

comments