Zaidi ya watoto 1,742 wenye umri chini ya miaka 15 wameugua surua na wanane kati yao kufariki kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2022 ambapo wazazi na walezi wamehimizwa kuwapeleka watoto wanaopaswa kuchanjwa na kupatiwa matone ya Vitamin A ili kutokomeza maradhi hayo yanayoweza kusababisha upofu, kupooza na hata kifo.

Hayo yamebainishwa hii leo Novemba 18, 2022 na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman katika eneo la Masingini Wilaya ya Magharib A wakati akizindua Chanjo ya Surua, Polio na utoaji wa matone ya Vatamin A, kwa watoto ili kuzuia na kudhibiti mripuko wa maradhi hayo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman (wa pili kushoto), wakati akipokea maelezo kuhusu wagonjwa wa Surua kutoka kwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya watoto Dokta Zubeida Mohammed Hussein (kulia) katika wodi ya wagonjwa wa surua iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja mjini ZaNzibar Oktoba 28, 2022.

Amesema, hatua hiyo ya kuendesha kampeni ya chanjo inatokana na uwepo wa maradhi hayo tangu Januari na mwezi Machi 2022 ambapo jumla ya wagonjwa 17,500 waliripotiwa katika visiwa vya Unguja na Pemba na kwamba watahakikisha wanazuia uingiaji wa Ugonjwa wa
Polio kama ilivyotokea kwa nchi za Msumbiji na Malawi.

“Wataalamu wa wizara ya Afya watahakikisha kupita nyumba kwa nyumba katika kampeni hiyo ili kuwachanja na kuwapatia matone ya vitamin A watoto wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 350,000 katika visiwa vya Unguja na Pemba na Serikali inafanya hivi kwa kutambua kwamba kinga ni bora kuliko tiba,” amesema Othman.

Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar, Dkt. Salim Nassor Slim wakati alipokuwa akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman kuhusu wagonjwa wa surua waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazuri suala la utoaji wa chanjo mbali mbali liliyumba mwaka 2020 baada ya kuzuka maradhi ya Uviko-19 na kwamba baada ya kudhibitiwa ugonjwa huo nguvu kubwa inaelekezwa katika chanzo za surua, Polio na utoaji wa matoni ya Vitamin A.

Awali, Mtalamu wa Chanjo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Wilium Mwenge amesema kwamba Mashirika na wadau mbalimbali wa Afya Duniani , wanaunga mkono juhudi za serikali za na kwamba kwa pamoja wataendelea kutoa ushirikiano katika jitihada za
kutokomeza ugonjwa huo.

Ruvu Shooting wakiri mambo magumu Ligi Kuu
Nelson Okwa aenguliwa Simba SC, Chama arejea