Mapigano nchini Syria yamesababisha vifo vya raia 250 ndani ya saa 48 za mapigano hayo yaliyoshika kasi zaidi juzi na jana.

Idadi hii ya mauaji ya raia ni kubwa zaidi ndani ya kipindi kifupi tangu mwaka 2013 ilipodaiwa kufanyika mashambulizi ya kutumia kemikali.

Kwa mujibu wa taasisi inayotazama vita hiyo kutoka Uingereza, raia 106 waliuawa Jumanne wiki hii katika mashambulizi yaliyotumia ndege za kivita kulenga makaazi ya raia pamoja na hospitali kadhaa.

Hospitali sita zilishambuliwa ndani ya siku mbili hali iliyosababisha nyingine tatu kufungwa, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Mashambulizi ya ndege za kivita yanayofanywa na Serikali ya Syria ikilenga maeneo yanayaoaminika kuwa makaazi ya waasi, yamesababisha hali ya taharuki kwa wakaazi wa Damascus.

Daktari wa Damascus, Khalid Abulabed ambaye yuko chini ya ulinzi wa majeshi mjini humo ameelezea hali hiyo kuwa ni hatari na isiyoelezeka.

Majeshi ya Syria yanayoungwa mkono na Urusi pamoja na marafiki zao yanaendesha mashambulizi dhidi ya waasi ambao wanaungwa mkono na Marekani, huku pande zote pia zikidai kupambana na kundi la kigaidi la ISIS ndani ya ardhi ya nchi hiyo.

Madonna amtabiria ‘mwanae’ urais wa Malawi
Prof. Mbarawa asema waliovamia hifadhi ya barabara hawatalipwa