Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema suala la ulinzi wa nchi ni la watanzania wote na sio la kuwaachia jeshi la wananchi, uhamiaji, poilisi au Magereza.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi wa Matogoro wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.

“Suala la ulinzi ni letu sote na sio la Serikali pekeyake kupitia wanajeshi au polisi. kila mtanzania anawajibika kulinda nchi hii, kuanzia nyumbani kwako hadi kwa jirani yako. Niwakumbushe kwamba tunapaswa tuendelee kujenga utamaduni wa kutoa taarifa kila unapoona kuna jambo ambalo una shaka nalo” amesema Waziri Mkuu.

Amebainisha kuwa mikoa ya pembezoni Kigoma, Kagera, Mtwara, Ruvuma, Katavi, Songwe, Mbeya, lindi, Mara, Tanga, Kilimanjaro, na Arusha ni mikoa ambayo wananchi wake ni lazima wawe wepesi kutoa taarifa.

Amesema Serikali imeweka mwongozo kwa wageni wanaoingia nchini ambao ni lazima apite kwenye mpaka ulio rasmi na kutoa taarifa zake ” mgeni huyo atapaswa aeleze amekuja nchini kufanya nini, amekuja na nani na atakaa kwa siku ngapi”

Ameongeza ” Tunapomupona mgeni huko kijijini, ni lazima tujiridhishe kuwa mgeni huyo amepitia kwenye sehemu zote husika. kama mtu utaona shaka, toa taarifa kwa mtendaji naye atapeleka taarifa hizo ngazi za juu hadi kwa Mkuu wa Wilaya”

Arsenal FC kumtoa sadaka Guendouzi
Ronaldo aifikia rekodi ya Giuseppe Signori