Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempa siku saba Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatoa kibali kwa kampuni ya BM Motors cha kutengeneza na kuunganisha bodi za magari.
 
Ameyasema hayo wakati akifunga maonyesho ya wiki ya Viwanda yaliyomalizika mkoa wa Pwani, katika Uwanja wa Sabasaba, Picha ya Ndege, Kibaha.
 
Amemtaka Waziri Mwijage, ifikapo Ijumaa wiki ijayo ampe taarifa ya maendeleo ya kampuni hiyo kuhusiana na kibali hicho kutoka TBS.
 
Aidha, amesema kuwa wakati mwingine huo ni urasimu, kama ana tatizo aambiwe ili aboreshe na hawezi awe amekaa tangu mwaka jana analalamika hajapata kibali cha kutengeneza mabodi.
 
“Na kwa nini msimpe hiyo fursa atengeneze bodi halafu mmwambie arekebishe na mkiwa mmejiridhisha kama ana uwezo wa kutengeneza hayo mabodi na Watanzania waendelee kutengeneza hapa nchini, badala ya kuagiza nje kwa gharama kubwa haina maana” amesema Majaliwa.
 
Hata hivyo, Majaliwa amesema kuwa, Mwijage alisema anaogopa kutumbuliwa sasa hamtumbui lakini mempa siku saba ili aweze kupata taarifa ya mwenendo wa kampuni hiyo.
 
  • Muro aanza kuwashughulikia vigogo waliopiga bilioni 3 za Kanisa
 
  • Wanaume waongoza kwa kujiua
 
  • LIVE: Msemaji wa Serikali akizungumza na waandishi wa habari
 
Mapema Waziri Mwijage akisalimia wananchi, alisema kwamba mashirika yaliyo chini ya wizara yake yakifanya kinyume yanahatarisha ajira yake, na yeye hayuko tayari kwa hilo.

Video: Waraka wa Zitto miaka mitatu ya JPM, Sakata la Sh1.5 trilioni laibuka upya
Raila atangaza kung’atuka siasa za kuwania urais 2022