Mchambuzi wa Soka la Bongo Willson Oruma ameonesha wasiwasi kwa Kocha Mkuu wa Simba SC Zoran Maki, na kuhisi huenda mambo yakamshinda kama hatafanya mabadiliko ya haraka kwenye kikosi chake.

Zoran Maki jana Jumatatu (Agosti 08) alicheza mchezo wa kwanza wa Kimataifa wa Kirafiki mbele ya Mashabiki wa Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa katika Tamasha wa Simba Day, SC na kukishuhudia kikosi chake kikiibuka na ushindi wa 2-0.

Oruma amesema pamoja na ushindi wa Simba SC katika mchezo huo, ameona kuna udhaifu katika safu ya Ulinzi na Ushambuliaji, hivyo kuna ulazima kwa Kocha huyo kutoka nchini Serbia, kurekebisha kwa haraka mapungufu hayo.

Amesema kama Kocha Zoran atashindwa kufanya hivyo kabla ya kukutana na Young Africans Jumamosi (Agosti 13) na kwa bahati mbaya akapoteza mchezo huo, ataanza kupoteza uaminifu kwa Viongozi na Mashabiki wa klabu hiyo ya Msimbazi.

“Nimeona ufundi wa mchezaji mmoja (SimbaDay) kile anachoweza kufanya, bado coaching. Sijaona Muundo mzuri kwenye kuzuia wala kwenye kushambulia. Kwa potential ya kikosi hiki (Simba),”

“Kocha Zoran Maki anapaswa kufanya jambo katika siku zilizobaki kabla ya kukutana na Young Africans, kama atashindwa kufanya hivyo na bahati mbaya akapoteza mchezo huo, atajipotezea uaminifu kwa Mashabiki na Viongozi wa Simba SC,”

Katika hatua nyingine Oruma amempongeza Kocha Zoran kwa kuonesha imani kubwa kwa Mshambuliaji Mzawa Habib Kyombo, baada ya kumpa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya St George ya Ethiopia

“Zoran Maki ameonyesha imani kubwa sana kwa Habibu Kyombo. Sio kwa bahati mbaya, Kyombo ana Kila Silaha ya kuwa mshambuliaji hatari na taifa likamtegemea. Unapaswa kufanya zaidi,onyesha arrogance kwamba Simba haikuwa bahati mbaya,ni Merit” amesema William Oruma

Simba SC iliyokua imeweka Kambi mjini Ismailia-Misri kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/23, itakutana na Young Africans Jumamosi (Agosti 13) Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii, ambao pia utatumika kama sehemu ya Ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

'Biometric' yashindwa kumtambua mgombea Urais Kenya, wasiwasi waibuka
Meddie Kagere: Nilikuja kama Mfalme, Ninaondoka kama Gwiji