Habari picha ya mazishi ya Mwalimu Verdiana Mujwahuzi  mama yake mzazi Erick Kabendera ambaye ni mwandishi wa  habari za uchunguzi na anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi,aliyezikwa leo katika Kijiji cha Kashenge halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.

Akiongoza ibada ya mazishi hayo padre Frutunatus Rutahywa amewaomba watanzania kuzidi kupendana,kuombeana mema maana hakuna aijuaaye saa wa siku ya kifo chake ambapo Marehemu Verediana Mujwahuzi alizaliwa feburuali 24 mwaka 1939 na enzi za uhai wake amelitumikia taifa kama Mwalimu.

Katika mazishi ya Mwalimu Verediana,marafiki wa familia wametoa salaamu  za pole kwa familia huku wakiomba falimia kuzidi kushikamana katika kipindi hiki cha majonzi ambapo baadhi ya waliotoa salamu hizo ni pamoja na Kiongozi mkuu wa chama cha siasa ACT Wazalendo Mhe.Zitto Z. Kabwe mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Mhe.Balozi Khamis Sued Kagasheki aliyewakuwa mbunge wa jimbo la Bukoba Manispaa, Rugemeleza Nshala Rais wa chama cha wanasheria Tanzania (TLS)

 

 

Mwili wa marehemu Mwalimu Verdiana Mujwahuzi ukipelekwa makaburini kwaajili ya mazishi

 

 

Padre Frutunatus Rutahywa akiongoza ibaada ya mazishi ya maremu mwalimu Mwalimu Verdiana Mujwahuzi

 

 

Uingereza yamgeuka Trump tishio la kupiga maeneo ya Iran
Dudu baya akalia kuti kavu

Comments

comments