Kiungo wa klabu ya Man City, Yaya Toure amesema wachezaji na mashabiki wanaweza kuumia kufuatia hatua ya shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuvunja kikosi kazi kilichoundwa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika soka.

Toure mwenye umri wa miaka 33, alikuwa mmoja wa wajumbe katika kikosi kazi hicho kilichoundwa mwaka 2013 kusaidia kutokomeza ubaguzi.

Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura amesema kikosi kazi hicho kilikuwa na kazi maalumu ambayo tayari wameshaimaliza.

Hata hivyo, hatua hiyo imekosolewa vikali na wadau mbalimbali, akiwemo Toure ambaye alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki wa CSKA Moscow Oktoba mwaka 2013.

Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast amesema hatua hiyo ya FIFA itaweza kuwaumiza mashabiki na wachezaji kama mipango sahihi isipowekwa.

Afya ya Samweli Sitta yadhoofika, apalekwa Ujerumani kwa matibabu zaidi
Jurgen Klopp Aota Ubingwa Wa PL