Nyota wa muziki nchini Nigeria, Yemi Alade, ametumiwa mwaliko wa kuhudhuria katika tamasha la utoaji tuzo za ‘Annual Grammy Awards’ ambazo zitatolewa Februari 12, mwaka huu.

Tuzo hizo za 59 zitatolewa kwenye ukumbi wa Staples Center jijini Los Angeles, Marekani, ikiwa ni mara ya kwanza kwa msanii huyo kuhudhuria tamasha hilo kubwa.

Hata hivyo, kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo aliweka wazi mwaliko huo na kuwashukuru wote ambao walimuunga mkono kwa mwaka 2016.

”Naamini nafasi hii nimeipata kutokana na kujituma kwangu mwaka 2016 pamoja na mashabiki wangu kuonyesha kunijali, ninawashukuru wote kwa kunijali na kupenda muziki wangu” alieleza Yemi

Masauni apiga marufuku sare za magereza na uhamiaji kushonwa uraiani
Darasa: Diamond ni zaidi ya simba