Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans wameendelea kutoa dozi kwenye ligi hiyo, baada ya leo Jumatano (Juni 22) kuichapa timu ya Polisi Tanzania mabao 2-0 katika mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Mzunguuko wa 28 kwenye ligi ikiwa Young Africans haijapoteza mchezo wowote, huku mshambuliaji wao Fiston Mayele akishindwa kupachika bao kwenye mchezo wa leo.

Mabao pekee ya Young Africans yamewekwa kimyani na Feisal Salum “Fei Toto” pamoja na Chico Ushindi ambapo mabao yote yamefungwa kipindi cha kwanza.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 23 2022
Meya wa jiji, watendaji wake wasimamishwa kazi