Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema Visa sita kati ya kila visa saba vya ugonjwa wa korona havingunduliwi barani Afrika kutokana na hesabu wanayoifanya kulingana ambayo inaangalia vifo vilivyorekodiwa na viwango vya vifo vya visa vya ugonjwa huo.

WHO inakadiria kuwa takwimu halisi ni milioni 59 lakini kufikia sasa ni visa milioni nane tu vya Covid vimerekodiwa na ili kukabiliana na hili, WHO imependekeza ukaguzi zaidi wa kijamii katika nchi nane zinazolenga kufikia watu milioni saba na upimaji wa haraka katika mwaka ujao.

Kwa jumla, watu pekee ambao wanapimwa ni wale wanaojitokeza kwenye vituo vya afya na dalili na wale wanaokusudia kusafiri nje ya nchi hii inamaanisha kuwa idadi kubwa ya visa vya watu wenye dalili ambazo hazionekani ipo na kusababisha maambukizi zaidi.

“Pamoja na upimaji wa kiwango cha chini , bado tunapofika katika jamii nyingi sana barani Afrika, Upimaji zaidi unamaanisha kutengwa kwa haraka, maambukizi kidogo na maisha zaidi kuokolewa kupitia hatua zinazolengwa,” amesema mkurugenzi wa WHO wa Afrika Dr Matshidiso Moeti.

Nchi zitakazoshiriki katika mpango huu ni Burundi, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Guinea Bissau, Msumbiji, Congo-Brazzaville, Senegal na Zambia.

Kumekuwa na upungufu wa visa vipya vilivyorekodiwa hivi karibuni, na WHO inasema kwa sababu ya viwango vya chini vya chanjo kwa kuwa Covid bado ni tishio kwa wengi.

Hukumu kesi ya Sabaya kutolewa leo, kinachojili Mahakamani
Matumizi ya dawa za kulevya yaongezeka nchini Tanzania