Mtayarishaji wa vipindi, na mzazi mwenza wa Ruge Mutahaba,  Zamaradi Mketema leo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameunga mkono kampeni ya kumchangia Mkurugenzi wa Vipindi vya Clouds Media, Ruge Mutahaba ambaye yupo Afrika Kusini kwa matibabu.

Kampeni hiyo yenye hash Tag ”Familia ya Ruge nje ya Mutahaba”.

Ambapo jana kwenye mahojiano na Clouds TV kwenye kipindi cha 360 mdogo wa Ruge, Mbaki Mutahaba ameeleza kuwa Ruge anasumbuliwa na tatizo la figo ambalo limepelekea matibabu yake kuwa ya gharama zaidi kuliko kawaida ambapo amesema kwa siku anaweza kutumia milioni 5 hadi 6 kwa ajili ya matibabu pekee.

Mapema leo Zamaradi Mketema ameunga mkono kampeni hiyo kwa kuwataka watu mbalimbali kutuma jumbe za faraja na wenye chochote kutuma kwenye namba ya mdogo wa Ruge, kwani gharama za matibabu ya Ruge zimekuwa kubwa sana kuliko kawaida.

Kwenye ukurasa wa Zamaradi ameandika.

”Mbaki Mutahaba ambae ni mdogo wa Ruge Mutahaba ameeleza kwamba ni wazi kwamba gharama za matibabu ya Ruge ni kubwa mno. Amesema Rais Dkt Magufuli na wengine walichangia lakini gharama  hizo ni kubwa kuliko kawaida. ”Gharama za matibabu kwa kule ni kubwa kwa siku inaweza kufika milioni 5 mpaka 6, kuna namba ambayo imeandikishwa kwa jina la mdogo wake, Kemilembe Mutahaba  0752 222 210 hiyo ndiyo namba ambayo watu wanaweza kutuma sms za pole, faraja na hata wengine ambao wangetamani kutuma chochote.” Mbaki Mutahaba.

Aidha Ruge amekuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi hasa katika sanaa ya muziki amesaidia wasanii wengi kuonesha njia akiwemo Barnaba Classic, Amin, Nandy, Ruby, Mwasiti na wamepata mafanikio makubwa.

 

Majaliwa amtumbua Mweka Hazina Kibondo
Video: Fahamu watu maarufu wanaotumia mashoto na tabia zao

Comments

comments