Wakazi wa kisiwa cha Zanzibar katika mji wa Mcheweni, wamegubikwa na hofu baada ya boti mbili zilizokuwa na watu nane kupotea baharini jana, hadi sasa watu hao wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha.

Tukio hilo limesababishwa na upepo mkali uliovuma kwa kasi katika kisiwa hicho na kupelekea kupotea kwa boti zote mbili na watu waliokuwa ndani yake.

Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na kamanda wa polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mohamed Shamim amesema licha ya juhudi zilizochukuliwa na Serikali pamoja na kamati ya uokozi bado watu hao hawajapatikana na hawana taarifa yeyote hadi sasa.

Miongoni mwa walikuwa ndani ya boti hizo ni Mohamed Makame, Omar Ali, Kombo Ali, Rashid Othman, Mwalimu Bosi Faki, Kombo Faki, Omar Kombo na Said Ali Omar.

 

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 25, 2019
Manispaa ya Ilala yatakiwa kuharakisha uundwaji wa kamati za walemavu