Wakulima wa zao la Muhogo kutoka Wilaya za Kakonko, Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, wameiomba Serikali iwasaidie namna ya kupata soko la zao la Muhogo kwa kile walichokieleza kwasasa wanauza zao hilo kwa hasara.

Wakulima hao wametoa ombi hilo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Luis Bura ambapo wamesema kuwa kinachowafanya kwa sasa kuuza zao hilo kwa hasara ni uwepo wa madalali, wanaojipangia bei.

Akizungumza na wakulima wa zao hilo kuhusu kero hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Luis Bura amesema kuwa kwasasa hawawezi kuamua lolote hivyo amewaomba wakulima hao wawaite wakuu wote wa wilaya hizo tatu ili waweze kujadiliana namna ya kutatua tatizo hilo.

“Kwasasa hatuwezi kuamua lolote, niwaombe wakulima mtuite wote kwa pamoja kutoka Wilaya tatu, ili kutatua changamoto hii kama Wanakibondo ili tuwe na sheria ya pamoja na ndugu zetu wa Kakonko, na Kasulu,”amesema Bura

Hata hivyo, mwishoni mwa mwaka jana Wakulima wa zao la korosho nchini, waliingia kwenye mgogoro wa bei ya bidhaa hiyo kufuatia kutokukubaliana na wafanyabiashara ambapo Wakulima waligoma kuuza zao hilo kwa bei ya hasara, mpaka Serikali iliopingilia kati.

 

Mabalozi wa Marekani waunga mkono mapenzi ya jinsia moja
PSSSF yawaneemesha Wastaafu 10,000

Comments

comments