Mshambuliaji kutoka nchini Argentina, Gonzalo Higuain anatarajiwa kukamilisha usajili wa kujiunga na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC akitokea SSC Napoli ndani ya saa 24 zijazo.

Higuain atakamilisha safari ya kisoka kutoka mjini Naples hadi Turin, kufuatia mazungumzo ya usajili wake kwenda vyema kati ya viongozi wa SSC Napoli na Juventus FC ambapo imeripotiwa kiasi cha Euro milioni 90 kimekubaliwa kama ada ya uhamisho.

Tayari ilikua inafahamika mshambuliaji huyo anaondoka Stadio San Paolo, lakini kitendawili cha wapi angeelekea ndio kilikua kinasumbua, kutokana na ukubwa wa ada yake ya usajili ambayo ilionekana kuzishinda baadhi ya klabu ambazo zilitajwa kuwa mstari wa mbele kumsajili.

Liverpool, Arsenal na Chelsea za nchini England zilitajwa katika usajili wa Higuain mwenye umri wa 28, kabla ya Juventus kujitokeza hadharani na kuonyesha dhamira ya kweli ya uhamisho wake.

Mustakabali Wa Roberto Mancini Kufahamika Leo
Mwendo Kasi kuburuzwa mahakamani kwa wizi wa nauli, madereva nao kukiona