Mara baada ya Maalim Seif kushindwa kesi yake dhidi ya Profesa Lipumba na kuamua kuhamia ACT Wazalendo, leo mwenyekiti wa chama hicho, Zitto Kabwe amefunguka kumpokea Maalim Seif pamoja na kumkabidhi kadi ya uanachama wa chama hiko.

Mbali na Maalim Seif Sharif Hamad kukabidhiwa kadi namba moja ya chama cha ACT-Wazalendo, wanachama wengine wa CUF waliokabidhiwa kadi ya chama hicho ni Juma Duni Haji na Ismail Jussa.

Zitto amefunguka kuwa kwa kilichofanywa na Maalim Seif wao kama vijana wamejifunza kitu kikubwa sana ikiwa ni pamoja na kuona umuhimu wa kujenga Demokrasia ya kweli na kujenga imani kwa watu ambao wanakuwa tayari kufanya lolote ilimradi kufika kule ambapo wanakubaliana kufika.

Zitto amesema ”Nchi hii ni yetu sote sio ya mtu mmoja na kakikundi kake, watanzania wanataka wafanye kazi na wafurahie matunda ya kazi yao, na hili ndio jambo ambalo tunakwenda kulifanya tutalifanya  Tanzania bara na tutalifanya Zanzibar na tutaiweka Tanzania kwenye ramani kwamba wananchi wanaweza kupata uongozi mbadala na uongozi huo unaweza kuleta mabadiliko ambayo wamekuwa wakiyatamani;”.

Aidha ametoa shukrani zake za dhati kwa viongozi mbalimbali wa chama kikuu cha upinzani Chadema, kwa kutumia muda wao kumpigia simu, wengine kutuma jumbe mbalimbali za pongezi huku wengine wakitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kupongeza hatua hiyo kubwa ya kihistoria ambayo viongozi wa ACT- Wazalendo na viongozi waandamizi wa CUF wameifikia pamoja.

Kwani juhudi za ujenzi na mshikamano wa vyama vya upinzani ni juhudi za lazima kutokana na changamoto ambazo vyama vya upinzani zinakutana nazo, ameongezea Zitto.

 

Wafanyabiashara ya viumbe pori wamlilia Magufuli
Koffi Olomide ahukumiwa kwa kumbaka mnenguaji wake

Comments

comments