Mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic anataka kubaki AC Milan maisha yake yote, wakati akiangalia uwezekano wa kuongeza mkataba na miamba hiyo ya mji wa Milan.

Mkataba wake ukiwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu, Ibrahimovic amefunga mabao sita katika michezo tisa ya Ligi Kuu msimu huu 2021/22.

Ibrahimovic ameonyesha kuimarika zaidi kwa kiwango chake tangu alipojiunga na AC Milan kwa kipindi cha pili Januari 2020 na Mshambuliaji huyo ameonyesha hana nia ya kuondoka pale San Siro.

“Nataka kucheza kwa muda mrefu kadri inavyowezekana,” amesema Ibrahimovic ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha AC Milan kilichoshinda kwa mara ya mwisho taji la Serie A msimu wa 2010-11.

“Hebu tuweke presha hapa kwa Milan kunipa mkataba mpya na nina matumaini ya kubaki Milan kwa maisha.”

“Bado nina malengo ambayo natakiwa kuyapata na nataka kushinda tena Scudetto.” amesema Zlatan alipohojiwa na Televisheni ya Rai

Geita Gold kumrudisha Haruna Niyonzima
Bodi ya ATCL yaonywa