Mashetani wekundu (Man Utd) wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Sweden, Zlatan Ibrahimovic ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu bingwa nchini Ufaransa PSG.

Man Utd wameonyesha nia hiyo, kwa kuwasilisha ofa kwa wakala wa Zlatan ya kutaka kumsajili kwa mkatana wa mwaka moja.

Man Utd wanaamini mshambuliaji huyo atakua chachu ya kufanikisha azma ya kurejesha heshima huko Old Traffold, endapo atakubali kujiunga nao kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kigezo kikubwa walichokitumia Man Utd cha kutaka kumsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja, ni umri mkubwa wa miaka 34 alionao Zlatan kwa sasa, kwa kuamini itakua kama wanacheza pata potea, endapo watamsajili kwa mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja.

Taarifa za ndani zinaeleza kwamba Man Utd watakua tayari kumlipa Zlatan mshahara wa Pauni lakini mbili na ishirini na tano (225,000) kwa juma, endapo atakubali kujiunga nao.

Hata hivyo tayari Man Utd wameanza kukutana na vikwazo vya kumpata Zlatabn, kufuatia kuweka hadharani pendekezo lake la kutaka kufanya kazi na aliyewahi kuwa meneja wake wakati akiwa Inter Milan, Jose Mourinho.

Msimamo huo wa Zlatan, unaonyesha hayupo tayari kusajiliwa Man Utd na kucheza chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Uholanzi, Louis van Gaal.

Zlatan Ibrahimovic, anasubiri kufanya maamuzi ya wapi atakapoelekea na kucheza soka lake kwa msimu wa 2016-17, huku akijivunia kuwa na historia  nzuri ya kutwaa mataji 13 katika nchi za Uholanzi, Italia, Hispania pamoja na Ufaransa.

Borussia Monchengladbach Waisubiri Ofa Ya Arsenal
Roy Hodgson Kutembelea Nyota Ya Leicester City Euro 2016