Taarifa za vyombo vya usalama, zimeeleza kuwa Ndege ya kivita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC imeingia katika anga la nchi ya Rwanda, katika hatua ambayo Vyombo vya usalama mjini Kigali vimetafsiri kitendo hicho ni uchokozi, huku DRC ikikanusha madai hayo.

Rwanda inasema, Ndege hiyo aina ya Sukhoi-25 ilitua kwa muda mfupi kwenye uwanja wa ndege Rubavu magharibi mwa nchi yake hapo jana Novemba 7, 2022 na kudai kuwa tayari imewasilisha malalamiko kwa serikali ya mjini Kinshasa.

Ndege ya kivita ya Kisasa aina ya A J-10CE (fighter jet) . si ya Jeshi la DRC. Picha ya AVIC

Hata hivyo, katika taarifa yake, Serikali ya Kongo imesema ndege yake haikuwa na silaha, na iliingia kimakosa kwenye ardhi ya Rwanda ilipokuwa ikipiga doria kwenye mpaka baina ya nchi hizo mbili.

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, bado zipo katika mvutano kuhusiana na waasi wa M23, na DRC inaituhumu Rwanda kuwaunga mkono waasi hao, huku Rwanda ikiikanusha na hivi karibuni Viongozi hao wapande hizo mbili walikutana kukubaliana ili kumaliza mgogoro.

Serikali yatoa taarifa hali za majeruhi ajali ya Ndege
Aliyeokoa abiria ajali ya ndege ajiunga na Jeshi