Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amefichua kwamba, klabu hiyo inahitaji kutuliza akili zaidi katika kipindi hiki kufuatia matokeo mabaya iliyoyapata kwenye mechi mfululizo.

Juzi Jumapili (Januari 07), ilishuhudiwa Arsenal ikiondolewa kwenye michuano ya Kombe la FA baada ya kufungwa nyumbani mabao 0-2 dhidi ya Liverpool.

Kabla ya hapo, ilijikuta ikipoteza uongozi wake katika msimamo wa Ligi Kuu England ndani ya siku sita mpaka kuangukia naasi ya nne.

Arteta amesema: “Nadhani tunahitaji kuanza upya, muda tulionao sasa ni mzuri wa kujjandaa na mapambano yaliyo mbele yetu.

“Kazi yangu kubwa ni kuongeza viwango vya wachezaji na uchezaji wa timu na kupata matokeo mazuri. Ninachowaomba mashabiki waendelee kutusapoti.”

Mshambuliaji Singida FG anautaka ufungaji bora
Watatu kusajiliwa Kagera Sugar