Klabu za Chelsea, Manchester United na AC Milan zote zinapambana kutaka kumsajili beki kisiki wa Nice, Jean-Clair Todibo, katika dirisha hili la Januari lakini mabosi wa Nice wanadaiwa kupambana kuhakikisha beki huyo anabaki hadi mwishoni mwa msimu.

Todibo mwenye umri wa miaka 24, anahitajika na timu nyingi kutokana na kiwango bora alichokionesha tangu kuanza kwa msimu huu, ambapo amekuwa na muunganiko bora na beki mwenzake wa kati Dante.

Hata hivyo, changamoto kubwa ni kiwango cha pesa ambazo timu zinazomhitaji kuweka mezani kumng’oa kwani mpunga ukiwa mwingi Nice haitaweza kumzuia beki huyo kuondoka.

Staa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu huu amecheza mechi 14 za michuano yote.

Awali Man United ilidaiwa ndio ilikuwa na nafasi kubwa ya kuipata huduma yake kutokana na ukaribu wa mmiliki wake wa sasa, Sir Jim Ratcliffe ambaye pia ndiye pia mmiliki wa Nice.

Msuva avunja ukimya usajili Young Africans
Kocha Guinea Bisau aweka malengo AFCON 2023