Timu ya Mashujaa FC ya Kigoma, imeweka rekodi ya kusajili wachezaji wengi katika kipindi cha dirisha dogo la usajili ikiwa imeingiza wachezaji saba kwenye kikosi chake mpaka sasa.

Mashujaa ambayo imeweka kambi yake jijini Dar es salaam kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zitazoanza kuchezwa tena katikati ya mwezi Februari baada ya kusimama kutokana na fainali za AFCON, imeonekana kufanya usajili wa wachezaji wengi kipindi hiki ili kurudisha moto iliyokuwa nao kipindi ipo Ligi ya Championship na mechi za kwanza baada ya kupanda.

Timu hiyo imewasajili wachezaji Nyeyezi Juma kutoka Inter Star ya Burundi, Emmanuel Mtumbuka (Stand United) inayocheza Ligi ya Championship, Mpoki Mwakinyuke, Samson Madeleke, Omari Abdallah (Prisons), Reliants Lusajo (Namungo) na Mlinda Lango Patrick Muntari.

Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Mohammed Abdallah ‘Bares’, amesema kuwa usajili wote umefanyika kwa manufaa ya klabu, hasa baada ya kuangalia mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi ambazo tayari wameshacheza.

TARURA kuanza usanifu wa Daraja Mikumi
CFO - AngloGold Ashanti atembelea GGML