Johansen Buberwa – Kagera.

Viongozi Mbalimbali wa Wilaya Bukoba  wakiwemo Madiwani, wa Chama cha Mapinduzi – CCM pamoja na Viongozi wa Wanawake, wamepatiwa semina  ya Mafunzo ya Manunuzi ya asilimia 30 ya fedha za umma, zinazotoka serikali kuu iliyoeneshwa na Omuka hub kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi – PPRA ili kuanuish makundi yaliyolengwa na kusimamiwa

kikamilifu.Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo ya siku mbili mjini Bukoba, Wakili Winfrida Samba ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa PPRA amesema mafunzo hayo yanafanyika  Mkoani Kagera kwa mara ya pili na wanatamani elimu hiyo isambae maeneo yote nchini.

Amesema, “Elimu hii inasaidia kuondoa changamoto ya ajira kwa watu wasio na ajira, inawasaidia wanchi kuwanyanyua kiuchumi pamoja na kuwazesha kupata mikopo na makundi yaliyolengwa nakuwa sehemu ya kuwawezesha kupata mikopo kwa kuunda vikundi wanawake asilimia 5,Vijana asilimia 10,Wazee asilimia 5 na Watu wenye ulemavu 10.”

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu,  Neema Lugangira amesema Serikali kupitia ofisi ya waziri Mkuu inawawezesha kuwapatia watu uelewa juu ya Manunuzi ya umma aslimia 30, na zoezi hilo litashuka katika Wilaya nyingine za Mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera, Fatma Mwassa amesema elimu waliyopata itasaidia Miradi mingi ya Halmashauri inapochukuliwa na kuendelea kutekelezwa kwa kufanya manunuzi kwa usahihi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Africa Freedom of Information Center, Gilbert Sendugwa kutoka Uganda amesema manunuzi kwa nchi za Afrika Ethiopia ina asilimia 36.2, Uganda 38.2, Rwanda asilimia 37, Kenya asilimia 48 na Tanzania ikiongoza kwa kuwa na asilimia 48.1 kwa kuwa tengea wanawake asilimia 5.

Wakitoa neno la shukrani, baadhi ya washiriki akiwemo Agripina Salvatory na Hamim Mahmoud wamesema mafunzo hayo yamewapa mwanga wa wa kuzielewa sheria za Manunuzi na itawasaidia kwenda kuunda vikundi, ili wapate mikopo.

 

GGML, Chemba ya migodi kuandaa Mitaala ya Watalaam uchimbaji
Gamondi afichua siri Young Africans