Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa ameanza utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Katibu itikadi na uenezi CCM, Paul Makonda, Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ikiwemo yale ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.

Katika utekelezaji huo, Wakazi mbalimbali wamejitokeza ili kutatuliwa kero zao, ambapo wengi wao walionesha kufurahishwa juu ya utaratibu huo ulioanzishwa, huku idara mbalimbali za Halmashauri na taasisi za Serikali wakihusishwa.

Malisa amesisitiza kuwa utaratibu huo utakuwa ni endelevu na mikakati imepangwa ili kuhakikisha Wananchi wanafuatwa katika maeneo yao ikiwemo katika kata zao, ili kuwasikiliza.

Hata hivyo, amewataka wakazi wa Wilaya ya Mbeya kuendelea kushirikiana na Serikali huku akiwasisitiza endapo watakuwa na changamoto, anawakaribisha kusikilizwa ili kuzitatua.

Simulizi: Kuwa mtoto wa nje ya ndoa ni zaidi ya mateso
Matumizi ya Teknolojia kuimarisha ukusanyaji wa mapato