Mwanaume mmoja (62), kutoka mji wa Magdeburg nchini Ujerumani, anadaiwa kwa makusudi au kwa sababu za kibinafsi kuamua kuchanjwa mara 217 chanjo za Uviko-19 ndani ya miezi 29.

Ushahidi wa matikio ya mtu huyo, ulikusanywa na Mwendesha Mashitaka wa Magdeburg, aliyeanzisha uchunguzi wa madai ya ulaghai, lakini hakufungua mashitaka ya jinai.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Erlangen-Nuremberg, wamemfanyia vipimo mbalimbali mwanamume huyo kuchunguza madhara ya kinga ya mwili.

Mwanamume huyo, hata hivyo anadaiwa kuwa hakuripoti madhara yoyote yanayohusiana na chanjo hizo akizochoma na wala hakukuwa na dalili kwamba amewahi kuambukizwa Uviko-19.

Hali si shwari Old Trafford
Sukari yawatokea puani wakazi saba wa Dar es Salaam