Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Hersi Said amesema anaamini Mamelodi Sundown ndio timu pinzani zaidi katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2023/24.

Young Africans imepangwa kukutana na Mamelodi Sundown katika Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, baada ya Droo iliyofanywa jana Jumanne (Machi 12), mjini Cairo-Misri.

Hersi amesema ameipokea kwa mikono miwili Droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hivyo ni jukumu lao kama viongozi kuhakikisha wanaiandaa timu yao kukabiliana na Mamelodi Sundown.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema lengo lao ni kuhakikisha Young Africans inakuwa na thamani kubwa kisoka Barani Afrika, baada ya kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita na msimu huu wapo Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Mipango yetu kwa sasa ni kujenga thamani kubwa zaidi Barani Afrika mwaka jana tumecheza fainali ya Kombe la Shirikisho, Mwaka huu tutacheza Robo Fainali dhidi ya Mamelodi, kwetu hii ni kipimo kikubwa”

“Licha ya ukubwa wa Mamelodi kuwa timu kubwa, tumejipanga tayari Kwa ajili ya kupambana na Mamelodi Sundown. Niwaombe Wananchi wajitokeze Kwa wingi kuisapoti Yanga maana tunaenda kuweka historia ya kufuzu hatua ya nusu fainali lakini haiwezi Kwa kuwa rahisi lazima ucheze dhidi ya timu nzuri”

May be an image of football and text that says "#TotalEnergiesCAFCL CAF. CHAMPIONS LEAGUE QUARTER FINAL னமம YOUNG AFRICANS MAMELODI SUNDOWNS"

“Hatujafika level ya juu lakini walau tumepiga hatua, Mamelod wametuzudi pakubwa lakini dakika 90 za nyumbani na ugenini zinatosha kuonyesha timu ambayo itafuzu”

“Mimi kwangu Mamelodi Sundown ndio timu pinzani zaidi kwenye mashindano ya CAF na tulipata taarifa kuwa walikuja na Scout wao kutazama mchezo wetu dhidi ya Al Ahly pale Cairo” amesema Hersi Said

Ifahamike kuwa Young Africans itaanzia nyumbani Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuikabili Mamelodi Sundown kati ya Machi 29 na 30, huku mchezo wa Mkondo wa pili ukipangwa kuchezwa Afrika Kusini kati ya April 5–6.

Makala: Changamoto za Wanawake zipatiwe ufumbuzi
Julio Kocha Mkuu Singida Fountain Gate