Inaitwa “Sarco”, kifupi cha sarcophagus, ni mashine iliyochapishwa kwa 3D iliyovumbuliwa na Mwanaharakati wa Euthanasia wa Australia, Philip Nitschke na mbunifu wa Uholanzi, Alexander Bannink ikiundwa katika mfumo wa jeneza linaloweza kutenganishwa, lililowekwa kwenye stendi ambayo ina mtungi wa nitrojeni.

Sarco imetengenezwa maalumu kwa kuua mtu bila maumivu, ambapo mtu yeyote ambaye anataka kufa basi ataingia ndani ya mashine hiyo na kubofya kitufe na kapsuli itakayotoa nitrojeni na kisha atasikia kizunguzungu kidogo lakini atapoteza fahamu haraka na kufa.

Nitschke, ambaye amepewa jina la “Dr Death” kwa kazi yake hiyo ya kubuni mashine hiyo, anasema waliweka kielelezo cha kifaa kwenye onesho, pamoja na seti ya miwani ya uhalisia pepe, ili kuwapa wageni hali halisi ya maisha ya jinsi ingekuwaje watakapoketi kwenye mashine hiyo, kabla ya kubonyeza kitufe.

Alipoulizwa kuhusu utata unaozunguka euthanasia na vikwazo vya kisheria, Nitschke alisema: “Katika nchi nyingi kujiua si kinyume cha sheria, ni kusaidia tu mtu kujiua. Hii ni hali ambapo mtu mmoja anachagua kubonyeza kitufe na kufa bila maumivu badala ya ya kugongwa na treni au kujirusha ghorofani.”

“Ninaamini ni haki ya msingi ya binadamu (kuchagua wakati wa kufa). Sio tu fursa ya matibabu kwa wagonjwa sana. Ikiwa una zawadi ya thamani ya maisha, unapaswa kuwa na uwezo wa kutoa zawadi hiyo wakati wa kuchagua kwako,” alisema Nitschke

Inaarifiwa kuwa, ndani ya mashine hiyo, mtu akishaingia na kujilaza mfumo wa kielektroniki hutambua na kisha hutoa sauti kwa kutumia spika zilizofungwa humo kumuuliza muhusika yeye ni nani, wapi alipo na kama anafahamu kitakachotokea, kisha baada ya majibu yote kwa usahihi mtu huyo hutakiwa kubonyeza kitufe kilichopo ndani ili kutimiza azma yake.

Kisha muziki mororo huanza kuimba na kumbembeleza muhusika ambaye husikia raha na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja kabla ya kupoteza uhai huku akisikia raha.

Hata hivyo, taarifa za awali zinaonesha kuwa mashine hiyo kwasasa inapatikana Nchini Uingereza na Ufaransa pekee kwani Mataifa hayo sheria zinaruhusu mtu kujiuwa na gharama za kulipia kifo ni Dola 1,000 kwa mtu mmoja na hulipwa kabla.

Meneja asimamishwa kazi, Usuaji mradi wamsikitisha Dkt. Biteko
Job: Tunaifahamu Mamelodi Sundowns