Nyota wa Singida Black Stars (Ihefu FC), Mkenya Elvis Rupia amesema ni suala la muda tu kwa kikosi hicho kuleta ushindani kwa vigogo wa soka nchini kutokana na ubora wanaoendelea kuuonyesha katika michezo yao mbalimbali.

Kauli ya nyota huyo inajiri baada ya kuiwezesha timu hiyo kufuzu Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, baada ya kuifungia bao moja wakati kikosi hicho kilipoichapa KMC mabao 3-0, juzi kwenye Uwanja wa Azamn Complex.

Rupia ambaye pia alichaguliwa mchezaji bora wa mechi hiyo amesema ni jambo zuri kwao kama wachezaji kufuzu hatua ya Robo Fainali huku akitoa angalizo kwa timu nyingine kujipanga vizuri pindi watakapokutana nao.

“Ukiangalia timu yetu kwa sasa unaona wachezaji wote wanapambana vizuri na naamini kwa umoja wetu ambao tunaendelea kuuonyesha tutafika mbali zaidi ya hapa, huu ni mwanzo tu, hivyo mashabiki wetu waendelee kutupa sapoti yao,” amesema.

Rupia aliyejiunga na timu hiyo katika dirisha dogo la Januari mwaka huu akitokea Singida Fountain Gate amekuwa na kiwango bora hadi sasa kwa sababu amefunga jumla ya mabao manne katika mashindano yote huku katika Ligi Kuu Bara akifunga matatu.

Kabla ya kutua Singida Septemba mwaka jana, Rupia alitokea klabu ya Police Kenya akikumbukwa zaidi, kwani ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Kenya msimu uliopita baada ya kupachika jumla ya mabao 27 akiwa na kikosi hicho.

Ihefu (Singida Black Stars) ilifika hatua hiyo ya l6 Bora baada ya kuifunga Mbuni ya jijini Arusha inayoshiriki Ligi ya Championship mabao 2-0, ikiungana na Namungo, Coastal Union, Geita Gold, Azam FC na Tabora United ambazo tayari zimeshafuzu Robo fainali.

Usuaji wa Mradi: Wasimamizi ujenzi wa Barabara waondolewa
Watanzania wamuenzi Sokoine kwa kufanya kazi: Dkt. B iteko