Manchester United wanaamini Mshambuliaji kinda wa timu hiyo, Alejandro Garnacho amejiweka mbali na ugomvi ambao ungetokea kati yake na kocha wa timu hiyo, Erik ten Hag baada ya nyota huyo kuungana mkono habari kwenye mtandao wa kijamii inayomkosoa kocha huyo.

Ingawa kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka ndani ya klabu hiyo bado mshambuliaji huyo anaweza kushughulikiwa na kocha huyo kutoka Uholanzi.

Mtandao wa kijamii ulimkosoa Ten Hag namna alivyokitathmini kiwango cha Garnacho kwenye sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bournemnouth Jumamosi (Aprili 13) na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina kuunga mkono habari hiyo.

Kwa mujibu wa ESPN, Garnacho haraka aliondoa alama hiyo ya kuonesha kuunga mkono kukosolewa kocha huyo, huku chanzo hicho kikisema hatua yoyote anayoweza kuchukuliwa chipukizi huyo inachukuliwa kuwa mambo ya ndani kwenye klabu hiyo.

Kwenye mchezo huo, Garnacho alifanyiwa mabadiliko wakati wa mapumziko baada ya kupokonywa mpira uliozaa bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji wa Bournemouth, Dominik Solanke. Bao la pili la Bournemouth lililofungwa na Justin Kluivert pia lilitokea upande wa kulia ambao alicheza Garnacho.

Alipoulizwa baada ya mechi hiyo kwanini alimfanyia mabadiliko Garnacho wakati wa mapumziko, Ten Hag alijibu: “Nafikiri tulikuwa kurekebisha upande wa kulia. Na tukucheza vizuri, tuliacha nafasi tukiwa kwenye umiliki wa mpira, tulikuwa kufanya mabadiliko kule,”

Ten Hag pia alisema Garnacho hakuwa sawasawa kabla ya kuchaguliwa kuanza mchezo huo.

Rais Samia kutunukiwa Udaktari wa heshima Uturuki
Ndumbaro: Tunajikita ujenzi wa viwanja AFCON 2027