Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Shakhtar Donetsk Sergei Palkin amemfunda Kocha Mkuu wa Chelsea Mauricio Pochettino, namna ya kumtumia Kiungo Mshambuliaji Mykhailo Petrovych Mudryk.

Mudryk alisajiliwa Chelsea Januari 15, 2023, kwa ada ya Pauni Milioni 62 sawa na Euro Milioni 70, na hadi sasa ameitumikia klabu hiyo ya jijini London katika Michezo 40 na kufunga mabao manne.

Palkin anaamini Pochettino hajafahamu namna ya kumtumia Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, na ndio maana anashindwa kuonesha makeke yake kama alivyokuwa Shakhtar Donetsk.

“Mudryk ni mchezaji bora wa Ulaya, mchezaji wa kipekee. Ninaamini makocha wanahitaji kujifunza jinsi ya kumtumia na jinsi wachezaji wenzake wanahitaji kucheza naye.

“Ninapotazama akiwa anacheza pale Chelsea, karibu mashambulizi yote yanashuka upande wa kulia, sio kushoto, hakuzoea kucheza kwa namna hiyo, hivyo kuna haja kwa kocha wake kujifunza namna ya kumtumia.”

“Katika klabu yetu tulitambua uwezo wake na kuwataka wachezaji wetu kumtumia kwa kiwango cha juu zaidi inategemea na makocha wanavyomchukulia na kumfundisha bado ni mdogo.”

“Wanahitaji kuwasiliana naye kibinafsi ili kumwonyesha udhaifu wake na kukuza nguvu zake. Anaonesha kiwango cha juu cha soka la Ulaya.”

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 18, 2024
Kalvin Phillips kurudishwa Leeds United